Wakati huo huo Beijing imesema kuwa itamuwekea vikwazo Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi kwa kukitembelea kisiwa hicho.
Uhusiano wa kidiplomasia umezidi kudorora Ijumaa, ambapo Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilifuatilia kwa kusema kuwa itaahirisha mazungumzo kati ya viongozi wa kijeshi wa Marekani na China na kusimamisha mazungumzo ya nchi mbili kuhusu hali ya hewa na usalama wa baharini.
Blinken amesema Washington imekuwa ikirudia na kuweka wazi kwa Beijing kwamba haitafuti kuwa na mzozo, wakati mvutano wa kidiplomasia ukiendelea kuhusu ziara ya Pelosi katika kisiwa hicho kinachojitawala ambacho Beijing inakitambua kama ni chake.
Wizara ya mambo ya nje ya china ilitangaza Ijumaa kwamba itaweka vikwazo dhidi ya Pelosi na familia yake kujibu kuhusu vitendo vyake vibaya na vya uchochezi.