China ilifyatua makombora 11 katika eneo la bahari kuzunguka kisiwa cha Taiwan leo hii, kwa mujibu wa serikali ya Taiwan ikiwa siku moja baada ya spika wa baraza la wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi kukamilisha ziara yake ambayo imeikasirisha Beijing.
Jeshi la China lilifyatua makombora ya Dongfeng katika eneo la bahari karibu na mwambao wa mashariki, kusini, na kaskazini wa Taiwan mchana wa Jumatano imesema wizara ya ulinzi ya Taiwan.
China hapo awali ilisema kwamba itafanya majaribio ya kijeshi na kuathiri maaeneo sita karibu na Taiwan, na yatakwenda mpaka Jumapili.
Hata hivyo, mazoezi hayo Alhamisi yaliongezwa kwenye kanda saba ambapo mazoezi yatasogezwa mbele zaidi katika siku kwa mujibu wa maafisa wa Taiwan.
Chombo cha habari cha China kimesema majaribio yalijumuisha makombora za masafa ya mbali na kawaida na matokeo yaliyo tarajiwa yamepatikana bila ya kufafanua.