Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, naibu waziri wa mambo ya kigeni wa China Xie Feng amelalamika vikali ziara ya Pelosi kwenye kisiwa hicho kinachojitawala, na ambacho China inadai kumiliki, wakati akifanya mazungumzo ya moja kwa moja na Burns.
Shirika la Xinhua limemnukuu Xie akisema kwamba, "Ziara hiyo ni ya kichokozi na kwamba mathara yake ni makubwa", akiongeza kusema kwamba China haitatazama tu bila kuchukua hatua. Ziara ya Pelosi ndiyo ya kwanza ya afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani ya Taiwan ndani ya miaka 25, na tayari imeongeza taharuki kati ya mataifa yote mawili yanayoongoza kiuchumi ulimwenguni, na kutajwa na Beijing kuwa ya kichokozi.
Xie ameonya kwamba Marekani italipia makosa yake, wakati akiomba Washington kuchukua hatua mara moja kuepusha mathara yalioletwa na ziara hiyo. Pelosi aliwasili Taiwan Jumanne jioni licha ya onyo kutoka Beijing.