Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:07

Beijing: Dhoruba Doksuri yaua wawili, mvua zaendelea kunyesha zikizoa magari na kufurika barabara


Dhoruba Doksuri yasababisha mafuriko katika viunga vya magharibi  vya Beijing, China.
Dhoruba Doksuri yasababisha mafuriko katika viunga vya magharibi  vya Beijing, China.

Katika viunga vya magharibi  vya Beijing, magari yalizolewa na maji Jumatatu wakati mvua zikiendelea kunyesha kwa nguvu tangu mwishoni mwa wiki na kuzigeuza barabara kuwa mito, na kuua watu wasiopungua wawili.

BEIJING —

Wakati huo huo mamia ya wakazi wa maeneo hayo wakiwa wamekwama, licha ya juhudi za uokoaji usiku kucha kuwaondoa maelfu ya watu waliokuwa majumbani mwao.

Mamia ya barabara zimefurika maji katika mji mkuu wa China, huku picha za video zilizobandikwa kwenye vyombo vya habari vya serikali zikionyesha magari ambayo yamezama nusu katika wilaya ya Mentougou yakisukumwa na maji yanayo kwenda kwa kasi wakati mabaki ya dhoruba Doksuri iliyoweka rekodi ya mvua kubwa katika mji wenye karibu watu milioni 22.

Miili miwili iligundulika katika mto mmoja wakati wa doria ya dharura iliyokuwa ikifanyika huko Mentougou huku waokoaji wakiwaokoa mamia kwenda maeneo mengine salama ya mji huo.

Mvua kubwa zaikumba wilaya ya Mentougou, Beijing on Julai 31, 2023.
Mvua kubwa zaikumba wilaya ya Mentougou, Beijing on Julai 31, 2023.

Mbali na Beijing, mvua kubwa zimeendelea kumiminika katika mji jirani wa Tianjin na pia jimbo la Hebei katika eneo takriban lenye ukubwa wa Uingereza kufuatia Doksuri, dhoruba iliyopungua nguvu kuwa ukali wake kuwa kimbunga wakati wa wikiendi.

Mito mitatu kati ya mitano ambayo inaungana kutengeneza bonde la mto Hazi iliongezeka na kufikia kina hatarishi Jumatatu. Baadhi ya nyumba zilichukuliwa na maji hadi katika mto Yongding, na takriban watu 55,000 waliokolewa kutoka majumbani mwao katika mji wa Baoding, vyombo vya habari vya taifa viliripoti.

Doksuri ni moja ya dharuba zenye nguvu kupiga China baada ya miaka kadhaa na kusababisha mafuriko yaliyoenea kote wakati wa wikiendi katika jimbo la kusini mwa Fujian, na kuwalazimisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG