Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:18

Hali ya sintofahamu imezuka China kuhusu mahala alipo Qin Gang


Qin Gang akiwa ameshikilia nakala ya katiba ya China mjini Beijing nchini China. March 7, 2023.
Qin Gang akiwa ameshikilia nakala ya katiba ya China mjini Beijing nchini China. March 7, 2023.

Wachambuzi wanasema mazingira ya kuondolewa kwake yatapunguza uaminifu wa ulimwengu nchini China na kuongeza hali ya sintofahamu ambayo hatimaye inaweza kudumaza mfumo wa utawala wa China

Maswali kuhusu hatma ya waziri wa zamani wa mambo ya nje wa China, Qin Gang bado hayajajibiwa baada ya serikali ya China ghafla kumtaja mteuliwa atakayeshika wadhifa wake, Wang Yi, hapo Julai 25.

Wachambuzi wanasema mazingira ya kuondolewa kwake yatapunguza uaminifu wa ulimwengu nchini China na kuongeza hali ya sintofahamu ambayo hatimaye inaweza kudumaza mfumo wa utawala wa China. Mfumo wa China unatia mashaka, Alfred Wu, mtaalamu wa siasa za China katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Singapore (NUS) aliiambia VOA.

Wakati ukaguzi na uwiano katika mfumo huo unatoweka, itailazimisha China kutegemea kabisa uamuzi wa mtu mmoja na kunaweza kuwa na mambo mengi ya kushangaza ambayo hatimaye yanaweza kuharibu mfumo. Kufuatia kuondolewa kwake ghafla kiongozi huyo, wizara ya mambo ya nje awali ilifuta taarifa zote zinazohusiana na Qin kutoka kwenye tovuti hiyo lakini ilipofika Ijumaa asubuhi kwa saa za huko baadhi ya rekodi zake za mkutano zilionekana tena.

Wachambuzi wanasema hiyo inaonyesha ukosefu wa uratibu kati ya idara tofauti za serikali na pia inaonyesha kuwa uongozi wa juu wa China bado unatathmini kesi ya Qin kama ni tatizo.

Forum

XS
SM
MD
LG