Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:19

Korea Kaskazini yakaribisha wajumbe kutoka Russia na China kwenye maadhimisho ya siku kuu ya Ushindi


Kiongozi wa Kim Jong Un akiwa na waziri wa
Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu mjini Pyongyang, Alhamisi
Kiongozi wa Kim Jong Un akiwa na waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu mjini Pyongyang, Alhamisi

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekaribisha wajumbe wa kijeshi kutoka Russia pamoja na wajumbe wa kisiasa kutoka China hivi leo ukiwa mkesha wa maadhimisho ya miaka 70 ya siku ya Ushindi.

Hafla hiyo imeonekana kuwa siku muhimu kidiplomasia baada ya miaka kadhaa tangu ilipozuia wageni kutokana na janga la corona. Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu na kiongozi wa kisiasa wa China Li Hongzhong wamewasilisha barua kwa Kim kutoka kwa viongozi wa mataifa yao, Vladimir Putin na Xi Jingping, kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo cha KCNA.

Chombo hicho kimeongeza kusema kwamba barua hizo zimepokelewa kwa furaha, wakati Kim akisifu urafiki wa miongo mingi na mataifa hayo. Wajumbe wanaozuru walialikwa kwenye utumbuizaji wa muziki usiku wa manane, ili kusherehekea ushindi uliyotangazwa na serikali dhidi ya uvamizi wa Marekani.

Vita vya Korea vya 1950-53 vinachukuliwa kuwa ushindi kwa Korea Kaskazini wakati vikielezewa nchini humo kwamba vilianzishwa na Marekani pamoja na washirika wake.

Forum

XS
SM
MD
LG