Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:44

Baraza wa Usalama la UN lakubali kuondoa kikosi cha ulinzi wa amani nchini DRC


Sehemu ya Jengo la Umoja wa Mataifa
Sehemu ya Jengo la Umoja wa Mataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne limepitisha kwa kauli moja azimio la kuanza kuondoa kikosi chake cha kulinda amani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Idara ya habari ya Umoja wa Mataifa imeandika katika mtandao wa kijamii wa X kuwa wanachama wake wote 15 walipiga kura kukubaliana na azimio hilo.

Rais wa Jamuhuri ya Kidemikrasia ya Congo Felix Tshisekedi alisema mwezi Septemba alipokuwa katika mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa aliiomba serikali yake iharakishe kuondoka kwa majeshi hayo ya kulinda amani na kuhakikisha yanaanza kuondoka mwisho wa mwaka.

Kikosi hicho kinachoitwa MONUSCO, kilichukua jukumu hilo kutoka operesheni ya awali ya UN mwaka 2010 ili kusaidia kuzima ukosefu wa usalama katika sehemu za Mashariki katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati, ambako makundi yenye silaha yanapigania maeneo na rasilimali.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni uwepo wa vikosi vya MONUSCO, vimekosa umaarufu kwa kile wakosoaji wanasema kushindwa kuwalinda raia dhidi ya makundi ya wanamgambo na kusababisha maandamano mabaya sana.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG