Pamoja na kulaumiwa kwa vifo vya watu wanaofikia 500,000 wakati wa utawala wake kwa miaka 8, baadhi ya watu wa Uganda walioshiriki katika mitandao ya kijamii katika kumbukumbu ya Idi Amin wamempongeza kwa “kuweka taifa lake mbele na kulipenda”.
Marehemu Idi Amin aliaga dunia Agosti 16, 2003 huko Jeddah, mji wa Saudi Arabia ambako aliishi kama mkimbizi wa kisiasa kwa miaka 20. Jumatano ilikuwa ni siku ya kumbukumbu kufuatia kifo cha mtawala huyo.
Katika maoni yao kwenye mtandao wa Facebook wa gazeti la Uganda, Daily Monitor, mmoja ya waliotoa maoni yao kuhusu kumbukumbu ya Idi Amin, Ssendagire amesema, “ na urithi aliotuachia ni ule wa kuwa ni kiongozi mzalendo kuliko wote katika nchi yetu ambaye hakuwahi kutokea.”
Kuthibitisha kauli ya Ssendagire, Ouma Okumu ameongeza “ni kiongozi bora kuliko wote Uganda.
Amesema wakati wa utawala wake hakukuwa na ufisadi, uvamizi wa ardhi, wawekezaji hewa na yale aliyotufanyia yatadumu milele. Mungu amweke mahali pema.