Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 19:53

Trump amerejea kuzilaumu pande zote za mgogoro wa Charlottesville


Rais Donald Truimp
Rais Donald Truimp

Rais Donald Trump amerejea tena kuzilaumu pande zote kutokana na ghasia za kibaguzi zilizotokea Jumamosi Charlottesville Virginia.

Baada ya taarifa ya Jumatatu ambapo aliwashutumu wenye sera za kinazi pamoja na wazungu wenye sera za kibaguzi bila kusema chochote kuhusu kundi la pili ambalo lilikuwa linapinga sera hizo.

Trump alikuwa kwenye jengo lake la Trump Towers mjini New York Jumanne wakati akzingumzia suala la kuimarisha miundomsingi ya taifa.

Lakini kikao hicho na wanahabari haraka kiligeuka kuwa chenye majibizano kati ya Trump na wanahabari waliotaka kujua ni kwa nini ilimchukua siku mbili kutumia maneno kama wenye sera za kinazi, Ku Klux Klan pamoja na wazungu wenye sera za kibaguzi.

Wakosoaji wake wanasema kuwa taarifa yake ya awali ilikua dhaifu na ilishindwa kulaani wazungu wenye sera za kibaguzi kwa kuwataja kuwa walihusika na ghasia.

XS
SM
MD
LG