Washambuliaji wa kundi hilo, lenye ushirikiano na kundi la kigaidi la al Qaeda, walivamia kituo katika kijiji cha Hawadley kwa kutumia bomu la kujitoa mhanga, la kwenye gari, na kisha kufyatua risasi, Kapteni Aden Nur, afisa wa kijeshi katika mji ulio karibu, aliliambia shirika la habari la Reuters.
"Tuliwatimua al Shaabab. Tulipoteza wanajeshi saba, akiwemo kamanda wetu," Nur aliambia Reuters. Al Shabaab walidai kuhusika na shambulio hilo katika taarifa, wakisema kuwa limewaua "askari wengi walioasi, pamoja na kamanda wao".
Kambi hiyo iko takriban kilomita 60 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, na ilitwaliwa kutoka kwa udhibiti wa al Shabaab mwezi Oktoba mwaka jana, na vikosi vya serikali, na wanamgambo wa ukoo, wanaoshirikiana na serikali.