Mohamud alikuwa akihutubia umati mkubwa kwenye kampeni iliyoandaliwa na serikali dhidi ya wanamgambo hao wenye uhusiano na Al-Qaeda uliofanyika kwenye uwanja wa michezo katika mji mkuu Mogadishu chini ya ulinzi mkali.
“Ninawaomba, wakazi wa Mogadishu, kati yenu wako waasi , kwa hiyo wafurushe. Wako katika nyumba zenu, ni majirani, katika magari yanayopita karibu yenu,” alisema.
Al-Shabaab imekuwa ikiendesha uasi mbaya dhidi ya serikali kuu inayoungwa mkono na jumuia ya kimataifa kwa miaka 15, ikifanya mashambulizi nchini Somalia na nchi jirani ambazo zlipeleka wanajeshi katika vita dhidi ya wanamgambo hao.