Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:55

Afrika isiwe uwanja wa kimkakati wa vita -AU


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (mstali wa pili kushoto) akiwa na viongozi na wajumbe kutoka nchi za Africa huko Addis Ababa, terehe 25 Mei 2023. Picha na Amanuel Sileshi / AFP.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (mstali wa pili kushoto) akiwa na viongozi na wajumbe kutoka nchi za Africa huko Addis Ababa, terehe 25 Mei 2023. Picha na Amanuel Sileshi / AFP.

Afrika haitakiwi kuwa "uwanja wa kimkakati wa kivita" kwa mataifa yenye nguvu duniani, wakati ikikabiliana na vitisho kadhaa vya amani na usalama wake, viongozi wa Umoja wa Afrika walionya siku ya Alhamisi.

Bara hilo lenye watu bilioni 1.3 limejikuta katikati ya mzozo wa ushawishi kati ya mataifa makubwa, ambao umeongezeka maradufu tangu uvamizi wa Russia nchini Ukraine miezi 15 iliyopita.

Wakati ambapo AU iliadhimisha kumbukumbu ya kuundwa kwa mtangulizi wake, Umoja wa Nchi za Afrika, siku kama hii mwaka 1963, Ukraine yenyewe ilitangaza kutaka kuimarisha uhusiano na Afrika.

"Katika muktadha huu wa kimataifa wa mapambano ya maslahi tofauti ya kisiasa, azma ya kila upande inatishia kuibadilisha Afrika kuwa uwanja wa kimkakati wa kivita, na hivyo kuanzisha vita mpya baridi," mwenyekiti wa Tume ya AU, Moussa Faki Mahamat alisema.

"Katika mchezo wa pata potea, ambako mafanikio ya wengine yatasababisha hasara kwa Afrika, ni lazima kupinga aina zote za matumizi ya vyombo vya nchi wanachama," aliongeza katika hotuba yake aliyoitoa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

Moscow inatafuta uhusiano wa kina wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi barani Afrika na Asia wakati Russia ikizidi kutengwa katika jukwaa la kimataifa kutokana na mzozo nchini Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, ambaye yuko barani Afrika, siku ya Jumatano aliyasihi mataifa kadhaa ya Kiafrika kuacha"kutoelemea upande wowote" katika vita hivyo.

Mwezi Februari, nchi 22 wanachama wa AU zilijiweka kando au hazikupigia kura azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililoitaka Russia kuondoka Ukraine.

Nchi mbili kati ya hizo -- Eritrea na Mali -- walipiga kura kupinga azimio hilo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG