Kiongozi mpya wa shirika la msaada la umoja wa mataifa anataka hatua madhubuti zichukuliwe katika kuweka kipaumbele jinsi pesa za shirika hilo zinavyotumika.
Kadhalika amekiri kwamba wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha katika kuwasaidia watu katika maeneo yaliyokumbwa na vita kama Gaza, Ukraine. Sudan na kwingineko.
Tom Fletcher mwanadiplomasia wa muda mrefu, aliyeingia ofisini mwezi uliyopita kama afisa wa maswala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, amesma kwamba shirika hilo linataka kuonyesha kwamba litatumia vyema raslimali zilizopo, hata kama migogoro ni mingi, na ya muda mrefu katika sehemu nyingi za dunia.
Ofisi ya kusimamia maswala ya kibinadamu inataka msaada wa dola bilioni 47 kuwasaidia watu milioni 190 katika nchi 32 kote duniani, ingawaje inakadiriwa kuna watu milioni 305 kote duniani wanahitaji msaada.
Amesema dunia inaungua na hatua zinahitajika kuzima moto huo.
Ofisi ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA, iliomba msaada wa dola bilioni 50 mwaka 2024 lakini ilipata asilimia 43 pekee, kufikia mwezi huu.
Kuna wasiwasi mkubwa kuhusu utawala wa rais mteule wa Marekani Donald Trump kuhusiana na mchango wa Marekani ambayo ni mfadhili mkubwa wa umoja wa mataifa, endapo ataendelea kutoa mchango wa kifedha na Fletcher amesema atakuwa Washington muda mwingi kufanya mazungumzo na utawala wa Trump.
Forum