Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 11:48

Mapigano yazuka Juba


Mapigano makali ya bunduki yalizuka Alhamisi jioni, katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, baada ya vikosi vya usalama kwenda kumkamata mkuu wa idara ya ujasusi kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, na kutolewa tahadhari kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Mapigano yalianza majira ya saa moja usiku kwa saa za huko, na kuendelea mfululizo kwa saa moja kabla ya kumalizika amesema ripota wa Reuters.

Tahadhari kwenda kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambayo Reuters iliona, ilieleza kwamba mashambulizi yalihusiana na kukamatwa kwa mkuu wa zamani wa idara ya taifa ya ujasusi ama NSS. Iliwataka wafanyakazi hao kujificha maeneo salama.

Mapema Oktoba, rais Salva Kiir, alimfuta kazi Akol Koor Kuc, ambayo aliongoza NSS toka nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka Sudan, 2011, na alimteua mshirika wake wa karibu kuongoza idara ya ujasusi.

Forum

XS
SM
MD
LG