Haya yanajiri mwaka mmoja baada ya Umoja wa Afrika kukubaliwa kama mwanachama wa kudumu wa G20, zamu ya Afrika Kusini kuwa usukani inaonekana kama fursa ya kusukuma maendeleo katika maeneo yenye sera muhimu kwa maendeleo ya bara la Afrika.
Rais Cyril Ramaphosa ametaja vipaumbele vya ukuaji wa uchumi shirikishi, usalama wa chakula, mabadiliko ya hali ya hewa na teknolojia ya akili bandia, huku maelezo yakitarajiwa wiki ijayo.
Afrika Kusini ni soko la nne linaloibuka mfululizo kutwaa urais wa G20, ambao unazunguka kila mwaka, baada ya Indonesia, India na Bŕazil, na Ramaphosa amesema nchi yake ingetaka kuendeleza kazi za watangulizi hao.
Marekani itachukua nafasi hiyo mwezi Disemba 2025 chini ya uongozi wa Donald Trump, ambaye utawala wake ujao umetishia kuweka ushuru mkubwa wa kibiashara kwa mataifa yakiwemo Canada, Mexico na China, jambo linalozua hofu ya vita vya kibiashara.
Forum