Pia ameangazia uungaji mkono wa Beijing wa mradi wake wa miundombinu wa kimataifa, na mpango wa pamoja wa teknolojia kusaidia kile kinachojulikana kama Mataifa ya Ukanda wa Kusini wa Dunia.
Rais Xi, amesema “Mpango wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Sayansi Huria,” utaongozwa na China, Brazil, Afrika Kusini na Umoja wa Afrika ili kuhakikisha maendeleo ya kiteknolojia yananufaisha mataifa yenye maendeleo kidogo na yanayoendelea.
Kwa mujibu wa shirika la habari la serekali ya China, Xinhua, Rais Xi, ameongeza kusema China inaunga mkono G20 katika ushirikiano wa vitendo kwa manufaa ya Ukanda wa Kusini wa Dunia.
China inatarajia uagizaji kutoka nchi zinazoendelea kufikia zaidi ya dola trilioni nane kati ya sasa na 2030
Forum