Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:50

UN yaomba G20 kuongeza ufadhili kwa nchi maskini kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa


Simon Stiell, Mkuu wa masuala ya hali ya hewa katika Umoja wa Matifa.
Simon Stiell, Mkuu wa masuala ya hali ya hewa katika Umoja wa Matifa.

Mkuu wa ofisi ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa Jumamosi aliyasihi mataifa ya G20 kushinikiza kuendelea kwa mazungumzo ya COP29 kuelekea makubaliano ya kuongeza fedha kwa ajili ya nchi zinazoendelea, akionya kuwa bado kuna "njia ndefu ya kwenda" katika suala hilo.

Wadau walikutana usiku kucha katika juhudi za kupunguza tofauti zilizopo katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa mjini Baku, Azerbaijan, kabla ya mawaziri kufika wiki ijayo kwa siku za mwisho za mkutano huo, lakini tofauti kubwa bado zipo.

Afisa huyo mwandamizi, Simon Stiell, aliomba viongozi wa mataifa ya Kundi la 20, ambalo linajumuisha chumi kubwa zaidi duniani na wachafuzi wakuu, kuzungumzia suala hilo watakapokutana Brazil Jumatatu.

"Viongozi wa G20 wanapoelekea Rio de Janeiro, dunia inatazama na kutarajia ishara kali kwamba hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni ajenda kuu kwa mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi duniani," alisema Stiell katika taarifa.

Baadhi ya nchi zinazoendelea, ambazo hazihusiki sana na uzalishaji wa gesi chafuzi duniani, zinataka ahadi ya kila mwaka ya dola trilioni 1.3 kusaidia kukabiliana na athari za hali ya hewa na kuhamia kwenye nishati safi.

Kiasi hicho ni zaidi ya mara 10 ya kile wafadhili, wakiwemo Marekani, Umoja wa Ulaya na Japan wanacholipa kwa sasa.

Forum

XS
SM
MD
LG