Beijing imekuwa ikijadiliana na EU ili kufuta ushuru na kuiona Ujerumani yenye uchumi mkubwa katika umoja huo na mshirika mkubwa wa biashara wa Beijing barani Ulaya, ikiwezesha kuchukua jukumu muhimu.
Katika mkutano wa Jumanne, kando ya Mkutano wa G20, mjini Rio de Janeiro, Brazil, Rais wa China Xi Jinping alimwambia Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, kwamba kwa upande wake Beijing, itaendelea kutoa fursa za masoko kwa makampuni ya Ujerumani, kwa mujibu wa taarifa za mkutano kama ilivyo tangazwa na shirika la habari la serikali ya China, Xinhua.
Forum