Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:04

Russia yasema uhusiano wake na Iran unazidi kuimarika


Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu (Kushoto) na mwenzake wa Iran Ali Akbar Ahmadian
Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu (Kushoto) na mwenzake wa Iran Ali Akbar Ahmadian

Uhusiano kati ya Russia na Iran umefikia kiwango kipya, licha ya upinzani kutoka kwa mataifa mengi ya Magharibi, Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu, alisema Jumatano wakati wa ziara yake mjini Tehran.

"Tunalenga shughuli mbalimbali zilizopangwa, licha ya upinzani kutoka kwa Marekani na washirika wake wa Magharibi," shirika la habari la Interfax lilimnukuu Shoigu akisema.

"Shinikizo la vikwazo kwa Russia na Iran linaonyesha ubatili wake, wakati ushirikiano wa Russia na Iran unafikia kiwango kipya."

Shoigu alikutana na afisa wa ngazi ya juu zaidi wa usalama wa Iran, Ali Akbar Ahmadian, siku ya Jumatano, na walizungumza kuhusu mada mbalimbali, hasa maendeleo katika eneo la Caucasus, kulingana na kituo cha habari cha Nour News cha Iran.

Shirika la habari la Tasnim la Iran limeripoti kuwa, Waziri huyo wa Ulinzi wa Russia pia alitembelea Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, au IRGC, Kikosi cha Wanaanga siku ya Jumatano, ambako alikutana na Mkuu wa Kikosi cha Wanaanga cha Walinzi wa Mapinduzi Amirali Hajizadeh, huku akionyeshwa ndege zisizo na rubani, makombora na mifumo ya ulinzi ya anga.

Forum

XS
SM
MD
LG