Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:16

Biden, Netanyahu wajadili masuala mbalimbali mjini New York


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na rais wa Marekani Joe Biden.
(Picha na Jim WATSON / AFP)
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na rais wa Marekani Joe Biden. (Picha na Jim WATSON / AFP)

Rais wa Marekani Joe Biden, Jumatano alikutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu mjini New York, kujadili upanuzi wa makazi ya Israeli katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Viongozi hao pia walijadili juhudi za kuufanyia mageuzi mfumo wa mahakama wa Israeli, ambao wakosoaji wanasema unatishia demokrasia ya nchi hiyo.

Kabla ya mkutano huo, Biden alikuwa amesema kwamba, wangejadili masuala magumu.

Rais huyo alisema: "Mazungumzo yanazingatia maadili ya kidemokrasia, ambayo ni nguzo muhimu mno ya ushirikiano wetu, ikiwa ni pamoja na kuifanyia ukaguzi mifumo yetu, na kuzingatia suluhisho litakalopelekea kuwa na mataifa mawili ya Israeli na Palestina, na kuhakikisha kuwa Iran, kamwe haipati silaha ya nyuklia."

Viongozi wa Israeli kwa kawaida hualikwa kutembelea White House mjini Washington ndani ya wiki chache, baada ya kuchukua madaraka, lakini Biden sasa anafanya mkutano wake wa kwanza na Netanyahu, miezi tisa baada ya waziri huyo mkuu, kuunda serikali yake ya mrengo mkali wa kulia. Misimamo mikali ya serikali ya Netanyahu, dhidi ya Wapalestina na juhudi za kupunguza mamlaka ya mahakama, zinaonekana kuwa sababu zilizopelekea Biden kucheleweshwa kwa mkutano huo.

Forum

XS
SM
MD
LG