Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:15

Iran yasema mabadilishano ya wafungwa na Marekani yatafanyika


Mwanamke mmoja akiiingia kwenye mlango ambao umefunikwa na picha inayoonyesha mateka wa Marekani na wafungwa ambao wanazuiliwa nje ya nchi, Jumatano, Julai 20, 2022, katika kitongoji cha Georgetown, Washington.
Mwanamke mmoja akiiingia kwenye mlango ambao umefunikwa na picha inayoonyesha mateka wa Marekani na wafungwa ambao wanazuiliwa nje ya nchi, Jumatano, Julai 20, 2022, katika kitongoji cha Georgetown, Washington.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanaani alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba Iran inatarajia dola bilioni 6 za ufadhili  zilizozuiliwa kutokana na  vikwazo vya Marekani zitahamishwa kutoka  kwenye kaunti za Korea Kusini hadi akaunti za nchini Qatar.

Iran ilisema mabadilishano ya wafungwa na Marekani yatafanyika Jumatatu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanaani alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba Iran inatarajia dola bilioni 6 za ufadhili zilizozuiliwa kutokana na vikwazo vya Marekani zitahamishwa kutoka kwenye kaunti za Korea Kusini hadi akaunti za nchini Qatar, na hivyo kufungua njia ya kuachiliwa huru kwa Wamarekani watano waliokuwa wanaashikiliwa nchini Iran na Wairani watano wanaoshikiliwa nchini Marekani.

Ripoti zinazowanukuu watu wanaolifahamu suala hilo zilisema Qatar iliijulisha Marekani na Iran kwamba fedha hizo zilihamishwa Jumatatu.

Hakuna uthibitisho wa haraka kutoka kwa maafisa wa Marekani.

Msemaji wa Baraza la Usalama la taifa huko White House John Kirby aliiambia VOA wiki iliyopita kwamba utawala wa Biden unatarajia mabadilishano hayo yatafanyika katika siku zijazo.

Forum

XS
SM
MD
LG