Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:18

Wamarekani 5 waachiliwa huru na Iran katika mabadilishano ya wafungwa yaliyoibua utata


Wamarekani walioachiliwa huru na Iran wawasili mjini Doha, Qatar.
Wamarekani walioachiliwa huru na Iran wawasili mjini Doha, Qatar.

Wamarekani watanoambao Marekani inasema walikuwa mateka na ambao walikuwa wamefungwa kwa miaka kadhaa nchini Iran waliachiliwa huru kufuatia makubaliano ya mabadilishano yaliyoibua utata yaliyosimamiwa  na Qatar.

Mabadilishano hayo yalifanyika baada ya dola bilioni 6 za Marekani, ambazo awali zilikuwa mali ya Iran, zilizoshikiliwa nchini Korea Kusini, kuhamishiwa kwenye akaunti za nchi hiyo nchini Qatar, huku Iran pia ikataka wafungwa wanke walio nchini Marekani waachiliwe huru.

Raia hao wa Marekani wanaojumuisha mfanyabiashara na mwanamazingira waliondoka Iran wakiwa katika ndege ya Qatar na kusindikizwa na ndugu wawili na balozi wa Qatar.

Baada yao kuabiri ndege kwelekea Qatar, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema;

"Leo hii, uhuru wao, uhuru wa Wamarekani hawa, waliofungwa kwa muda mrefu sana na kuwekwa kizuizini nchini Iran bila haki, unamaanisha mambo ya msingi sana: una maana kwamba waume na wake, baba na watoto, babu na bibi, wanaweza kukumbatiana tena, wanaweza kuona kila mmoja. Wanaweza kuwa na kila mmoja tena."

Mpango huo wa ubadilishanaji wa wafungwa ulifikiwa kwa upatanishi wa Qatar.

Katika tukio ambalo lilitazamwa kwa makini kote duniani, Iran ilitaka kuachiliwa kwa fedha zake takribani dola bilioni 6 za kimarekani na kisha fedha hizo kuhamishiwa katika benki za Tehran nchini Qatar, huku ndege ya kuwabeba wafungwa hao ikiwa tayari muda wote mjini Tehran.

Baadhi ya wafungwa walipowasili mjini Doha, Qatar.
Baadhi ya wafungwa walipowasili mjini Doha, Qatar.

Kufuatia kufikiwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa mwezi uliopita, Wafungwa hao watano wa Marekani wako pia na uraia wa Iran, nchi ambayo haitambui uraia pacha, waliachiwa baada ya kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani.

Je wafungwa hao ni nani?

Ingawa baadhi hawakutaka majina yao yatajwe kwa hofu za kiusalama, Kati yao ni mfanyabiashara Siamak Namazi, mwenye umri wa mika 51, aliyekamatwa mwaka 2015 kwa mashtaka ya ujasusi ambayo familia yake iliyakataa.

Wengine ni mwanamazingira Morad Tahbaz, mwenye umri wa miaka 67, ambaye pia ana uraia wa Uingereza, mwekezaji Emad Sharqi, mwenye umri wa miaka 59, na wengine wawili ambao hawakutaka kutajwa majina yao.

Marekani imesema raia wake walifungwa kwa mashtaka yasiyo na msingi kama mtaji wa kisiasa.

Kuachiliwa kwa fedha hizo zilizokuwa zimefungiwa na mshirika wa Marekani Korea Kusini chini ya vikwazo vya muda mrefu ilikuwa ni sharti kuu la Iran kuwaachia wafungwa watano wa Kimarekani na Marekani pia kufanya vivyo hivyo kwa wafungwa watano wa Iran.

Abdullahi Boru, mchambuzi wa siasa za kimataifa ambaye amekuwa akifuatilia suala hili kwa mika kadhaa, na hasa sana miezi ya hivi karibuni baada ya Marekani kutangaza kwamba ilikuwa inajadiliana na Iran kuhusu uwezekano wa kubadilishana wafungwa, anasema mchakato huo ulikuwa unafanyika katika ngazi za juu zaidi za kidiplomasia.

"Qatar ilikuwa mpatanishi kwa sababu Tehran na Washington hazina uhusiano wa kidiplomasia," alisema Boru katika mahojiano na Sauti ya Amerika.

Wakati zoezi hilo la kuwaachia wafungwa likiendelea, rais wa Marekani Joe Biden ametangaza vikwazo dhidi ya rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad na wizara inayohusika na ujasusi.

Walisafirishwa hadi Qatar na baadaye kuabiri ndege ya kuwaleta hapa Marekani.

"Sina kipaumbele cha juu zaidi, rais hana kipaumbele cha juu zaidi ya kuhakikisha kwamba Wamarekani ambao wanazuiliwa isivyo haki popote wanaweza kurudi nyumbani. Tutaendelea na kazi hiyo siku zijazo," Blinken alisema.

Wairan walioachiliwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters ni Mehrdad Moin-Ansari, Kambiz Attar-Kashani, Reza Sarhangpour-Kafrani, Amin Hassanzadeh and Kaveh Afrasiabi.

Forum

XS
SM
MD
LG