Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:31

Marekani kufuatilia jinsi Iran itakavyotumia fedha za makubaliano ya kubadilishana wafungwa


John Kirby, msemaji wa masuala ya usalama wa kitaifa katika White House.
John Kirby, msemaji wa masuala ya usalama wa kitaifa katika White House.

Marekani imeahidi kufuatilia kwa karibu namna Iran itakavyotumia dola bilioni 6 zilizokuwa zimeshikiliwa ikiwa sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa, baada ya Rais wa taifa hilo Ebrahim Raisi kusema kwamba ni juu ya Tehran kuamua fedha hizo zitakavyotumika.

“Iwapo Iran itajaribu kutumia fedha hizo visivyo, hatuna budi kuzishikilia tena,” amesema John Kerry mratibu wa kitaifa wa Baraza la Usalama kwa ajili ya mawasiliano, wakati akitoa hotuba yake kwenye Ikulu ya Marekani.

Fedha hizo zilishikiliwa na Marekani kama sehemu ya vikwazo lakini sasa zitahamishwa kutoka kwenye akaunti iliyopo Korea Kusini hadi kwenye nyingine iliyopo Qatar.

Kirby amesisitiza kwamba fedha hizo hazitatolewa zote kwa mara moja, wala kuachiliwa bila masharti.

Kirby amesema kwamba Iran itakuwa ikitoa ombi la kutoa fedha kwenye akaunti kwa ajili ya matumizi ya kibinadamu pekee, na kwamba kutakuwa na uangalizi wa kutosha kuhakikisha hilo linafanyika.

Forum

XS
SM
MD
LG