Wanawake hao wajasiriamali wamekutana Jumatano jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimu mafunzo ya takribani wiki 14 yenye lengo la kuwapa elimu juu ya matumizi ya teknolojia katika kukuza biashara zao pamoja na kuwapa fursa za masoko katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mjasiriamali wa Tanzania aeleza jinsi mafunzo ya jukwaa la AWE yalivyomsaidia
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umewakutanisha wanawake wajasriamali zaidi ya 100 kutoka mataifa ya Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda kupitia jukwaa la Academic Women Enterpreneur (AWE) linalofadhiliwa na serikali ya Marekani, ili kuwapa mafunzo ya kuboresha uendeshaji wa biashara na makampuni.