Xi huenda akatawala China hadi kifo - Wachambuzi

Kamati mpya ya Politburo mjini Beijing, akiwemo Rais Xi Jinping.

Rais wa China Xi Jinping, ambaye Jumapili alithibitishwa tena kuwa katibu mkuu wa chama tawala cha Kikomunisti na mkuu wa majeshi na hivyo kupata muhula wa tatu kuongoza taifa lenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, amepata udhibiti kamili wa Chama cha Kikomunisti cha China.

Hata hivyo, wataalam wanaonya kwamba nguvu zake zisizodhibitiwa ni hatari kubwa, hususan wakati akikabiliwa na changamoto za kiuchumi na mvutano na Marekani.

Xi, ambaye alichukua madaraka mwaka 2012, alitunukiwa muhula wa tatu wa miaka mitano, tofauti na desturi ambapo, kwa mfano, mtangulizi wake aliondoka uongozini baada ya miaka 10.

Viongozi wa Korea Kaskazini na Russia, ni kati ya waliotuma risala za pongeza kwa Xi kwa kupata muhula wa tatu kama kiongozi wa chama cha kikomunisti cha China.

Wachanmbuzi wanasema kwamba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69 anatarajiwa na baadhi ya watu kujaribu kusalia madarakani maisha yake yote.