WHO imesema inaweza kusababisha mkanganyiko na kuwa na athari kubwa katika biashara na usafiri.
Afrika CDC imesema inasukuma kuwa na jukumu lenye nguvu katika kusaidia kudhibiti kusambaa kwa magonjwa kwa haraka zaidi.
Kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu pekee wa WHO, Tedros Adhanom ndiye anayeweza kutangaza dharura ya kiafya yenye wasi wasi wa kimataifa.
Afrika CDC inataka kulenga Afrika peke yake. Mkuu wa WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti anasema tangazo kama hilo linaweza kuwa na athari kubwa kwa nchi za Afrika.
Ametolea mfano wa dharura iliyojitokeza mwaka jana ya mlipuko wa kirusi cha OMICRON ambapo ilisababisha nchi za magharibi kulitenga bara la Afrika kwa kuliwekea vikwazo vya kusafiri.
Mapema mwaka huu, Malawi na Msumbiji walitangaza milipuko ya virusi vya polio kufuatia vifo vya watoto wawili katika nchi hizo za kusini mwa AFrika.
Mwezi Mei, Sierra Leone pia ilitangaza mlipuko wa anthrax.