Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 11:50

Maambukizi ya Covid yaongezeka maradufu Nigeria


Mwanamke afanyiwa vipimo vya corona mjini Abuja, Nigeria.
Mwanamke afanyiwa vipimo vya corona mjini Abuja, Nigeria.

Idadi ya maambukizi mapya ya covid 19 kila siku nchini Nigeria yameongezeka maradufu kufikia Jumatano na kupanda zaidi ya 4,000, ikiwa idadi kubwa zaidi tangu kuzuka kwa janga hilo.

Maafisa wa afya nchini humo wamesema kwamba hali hiyo inatia wasiwasi hivyo kuwasihi watu kujiepusha na mikusanyiko. Idadi hiyo imetangazwa wakati Nigeria ikiwa imetupa dozi milioni moja ambazo muda wake wa matumizi ulikuwa umekaribia kumalizika.

Idadi hiyo ya karibuni iliyotangazwa Alhamisi ni karibu mara mbili ya ile ya siku iliyotangulia.Wataalam wa afya wanasema kwamba ongezeko hilo linaashiria kuingia kwa wimbi la nne la mambukizi nchini humo yakihusishwa na aina mpya ya virusi vya omicron.

Ifedayo Adetifa ambaye ni mkuu wa kituo cha kitaifa cha kudhibiti magonjwa,CDC Nigeria, amesema kwamba tabia ya virusi vya corona imepitia mabadiliko mengi na moja wapo ni kwamba aina mpya ya virusi vinasambaa kwa haraka.

Tangu Februari mwaka 2020, Nigeria imetangaza jumla ya kesi 230,000 za maambukizi kutokana na virusi vya corona.Kituo cha CDC kimewashauri watu dhidi ya kufanya safari wakati huu wa sikukuu ili kuzuia kenea kwa maambukizi.

XS
SM
MD
LG