Siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu wa taifa la kisiwa kidogo cha Barbados alitoa hotuba yenye kusisimua katika baraza hilo, akihoji nani atasimama kuwapigania watu kote duniani na kutekeleza hatua zinazohitajika sana.
“Kwa maneno ya Robert Nestor Marley, nani atanyanyuka na kusimama kidete ?” Waziri Mkuu wa Barbados Mia Amor Mottley aliwauliza viongozi waliokusanyika katika mkutano wa mwaka, akimnukuu muimbaji maarufu wa Jamaica. “Nani atasimama na kupigania haki za watu wetu?”
Akisoma hotuba kutoka katika simu yake ya kiganjani, waziri mkuu huyo alipitia orodha ndefu ya changamoto ikiwemo ukosefu wa uwiano katika usambazaji wa chanjo ya COVID-19, ukosefu wa ajira, masuala ya usafirishaji na mbadiliko ya hali ya hewa.
Alisema siyo nje ya jumuiya ya kimataifa kutatua hayo; ni kwamba viongozi wamechoka kukabiliana na matatizo haya kila mwaka na hawaoni kinachobadilika.
“Kama tuliweza kuwa na nia thabiti ya kupeleka watu kwenye mwezi na kupata ufumbuzi wa vipara vya wanaume, kama nilivyosema mara kwa mara, tunaweza kutatua matatizo mepesi kama vile kuwawezesha watu wetu kumudu kupata lishe na kuhakikisha tuna usafiri,” amesm
Viongozi wanawake walikuwa wachache wiki hii, wakiwa ni chini ya moja ya kumi ya wazungumzaji hadi sasa. Uhaba wao katika nafasi za madaraka unabanisha vikwazo wanavyokabiliana navyo wanawake katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea kuweza kufikia nafasi za juu za uongozi katika serikali.
Mzozo wa hali ya hewa umekuwa ni kauli mbiu muhimu inayojirejea wiki hii. Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Rebecca Nyandeng de Mabior amesema imewaathiri watu Kariba 800,000 katika nchi yake.
De Mabior alisema kuwa “mvua kubwa”zimesababisha mafuriko mabaya sana katika miaka 60 na kuzamisha vijiji, miji, ardhi na mifugo.
“Hivyo basi, wito wangu kwa jumuiya ya kimataifa wasaidie kuokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 5.5 wanaohitaji misaada ya kibinadamu,” aliongoza.
Wakati nchi nyingi duniani zikiwa zinahangaika na janga la COVID-19, athari zake huko New Zealand sio mbaya sana kwa sababu viongozi wake walichukuwa tahadhari mapema kudhibiti virusi hivyo.
Nchi hiyo ina maambukizi yaliothibitishwa zaidi ya 4,000 na vifo 27, kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, kinachofuatilia janga hilo ulimwenguni. Pia New Zealand iko katika kampeni ya chanjo ya kitaifa.