Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:53

Marekani kutoa chanjo za ziada za Covid milioni 500


Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York

Marekani inajianda kutoa msaada wa chanjo za ziada millioni 500 za Covid 19 za Pfizer kwa mataifa kadhaa kote duniani, na hivo kufikisha jumla ya  dozi billioni moja kufikia sasa.

Jumatano, Rais Joe Biden atakuwa mwenyeji wa mkutano kwa njia ya mtandao kuhusu janga la Covid 19 na anatarajiwa kutangaza ahadi hiyo ya dozi millioni 500 za chanjo.

Mapema Jumanne, Biden aliambia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa mjini New York kwamba Marekani imetenga zaidi ya dola billioni 15 kwenye mpango wa kimataifa wa kukabiliana na Covid 19 ili kufadhili zaidi ya dozi millioni 160 za chanjo ya covid 19 kwa nchi nyingine.

Marekani ilinunua dozi millioni 500 za Pfizer na imezitoa kama msaada kupitia mpango wa COVAX.

Biden amesema chanjo hizo zimekwisha wasili katika nchi 100, akiongeza kuwa atatangaza ahadi za ziada Jumatano kwenye mkutano kuhusu Covid 19 ambao Marekani ni mwenyeji.

Marekani inawashinikiza viongozi wa dunia kuidhinisha malengo yao ya kutokomeza janga la covid 19, na kuhakikisha kwamba asilimia 70 ya watu ulimwengu wamechanjwa ifikapo mwaka wa 2022, kulingana na waraka wa Marekani ambao Reuters imeuona.

XS
SM
MD
LG