"Hatuwezi kuokoa sayari yetu ikiwa tutawaacha walio katika mazingira magumu - wanawake, na wasichana wachache," Rais wa Slovakia Zuzana Caputova aliambia mkutano mapema wiki hii.
"COVID-19 inatishia kurudisha nyuma mafanikio ambayo tumepata," Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, rais wa kwanza mwanamke wa nchi yake, aliuambia mkutano Baraza Kuu la UN Alhamisi.
Siku hiyo ya Alhamisi pia, Katibu Mkuu wa UN, António Guterres, alionya katika mkutano wa chakula ambao unataka kuboresha uzalishaji wa chakula ulimwenguni kwamba karibu nusu ya dunia haiwezi kumudu chakula bora.
"Chakula ni uhai. Lakini katika nchi, jamii na kaya katika kila kona ya ulimwengu, hitaji hili muhimu - haki hii ya binadamu - halijatimizwa," Guterres aliuambia Mkutano wa Mifumo ya Chakula pembeni mwa mkutano huo wa kila mwaka.
Guterres alisema kuwa watu bilioni 3 hawawezi kumudu chakula chenye lishe. "Kila siku, mamia ya mamilioni ya watu hulala na njaa. Watoto wanakufa na njaa," alisema.
Wakati mamilioni ya watu wanakufa njaa, na athari za njaa zinajidhihirisha wazi katika nchi kama Yemen na Ethiopia, karibu theluthi moja ya chakula chote kinachozalishwa hupotea au kuharibika.