Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, ziara ya mwisho ya waziri wa mambo ya kigeni wa Iran nchini Misri ilikuwa ya Ali Akbar Saleni, mnamo 2013 mjini Cairo. Araghchi ambaye yupo kwenye ziara za mataifa kadhaa aliwasili Cairo baada ya kutembelea Jordan, alipokutana na kuzungumza na mwenzake Ayman Safadi.
Wawili hao walizungumzia masuala ya maendeleo ya kieneo wakati “ kukiwa na ukatili na uchokozi dhidi ya Gaza na Lebanon”, kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Iran Esmaeli Baghaei. Araghchi wakati akiwa Jordan pia alikutana na mfalme Abdullah wa Pili mjini Amman.
Ndani ya wiki moja iliopita, Araghchi ametembelea Lebanon, Syria, Saudi Arabia, Qatar, Iraq na Oman, ikiwa juhudi ya kupunguza taharuki pamoja na kudhibiti mzozo wa Mashariki ya Kati kuenea. Baadaye kiongozi huyo atatembelea Uturuki na Misri kulingana na wizara yake.