Waziri huyo alisema kuwa ni wakati kwa Ulaya kutathmini upya vikwazo dhidi ya Damascus kwa kuwa hali ya kisiasa imebadilika. Alhamisi akiwa mjini Rome aliongoza mkutano na maafisa wa wizara za mambo ya nje kutoka chini tano- Uingereza, Ujerumani, Italy na Marekani, wakati awali akizungumza kwa njia ya simu na wenzake wa Uturuki na Saudi Arabia.
Alisema lengo kuu ni kuratibu miradi baada ya kuondoka kwa Assad, na kwamba Italy ipo tayari kufanya mapendekezo ya uwekezaji binafsi kwenye sekta ya afya kwa ajili ya watu wa Syria. Wakati wa kikao cha Rome ambacho waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alihudhuria, Tajani alisema kuwa ni muhimu kwamba watu wote wa Syria watambuliwe kuwa na haki sawa.
Hilo ni kutokana na wasi wasi kuhusu haki za Wakristo pamoja na makundi mengine ya walio wachache, chini ya utawala mpya wa kundi la Hayat Tahrir al Sham, au HTS, kundi la Kiislamu ambalo kwa muda mrefu likitajwa la kigaidi na Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa.