Viongozi wa wanamgambo wanaopinga jihadi wamelilaumu kundi la Islamic State la Afrika magharibi (ISWAP) kwa shambulizi la wiki iliyopita katika jimbo la BORNO eneo ambalo lina uasi mkubwa wa wana- jihadi ambao wamesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 na kuwakosesha makazi wengine milioni mbili tangu mwaka 2009.
Taarifa za kina kuhusu shambulizi katika eneo la vijijini la ngala bado hazifahamiki na maafisa wametoa taarifa zinazokinzana. Idadi ya watu walioripotiwa kuwa hawajulikani walipo hailingani na ile ya watu wanaoshikiliwa mateka.
Ofisi ya umoja wa mataifa inayoshughulika na masuala ya kibinadamu – OCHA imesema shambulizi lilifanyika alhamisi wiki iliyopita na inakadiriwa kuwa watu 200 kutoka kwenye kambi za waliokoseshwa makazi wametekwa.
Imesema washambuliaji waliokuwa na sialaha waliwateka wanawake wakiwa nje wanatafuta kuni.