Rais Bola Tinubu ailitoa amri ya uchunguzi wa kina ufanyike kufuatia shambulio hilo, ambalo liliwalenga wanamgambo na majambazi.
Jeshi la nchi kavu na lile la anga yalitakiwa kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka katika majimbo ya kaskazini-magharibi na kati, yanayotishiwa na magenge ya wahaliufu wenye silaha ambayo huwashambulia kwa risasi wakazi wa vijiji na kuwateka nyara. Jeshi pia linapambana na wanamgambo wa kiislamu huko kaskazini maskariki ya nchi.
“Tuko hapa kuwalinda raia wasio na hatia, siyo kuwashambulia. Kulikuwa na makosa, na kunayafanyia kazi matatizo hayo” Jenerali Musa aliwaambia waandishi wa habari huko Abuja.
“Ripoti iko tayari na itatolewa labda kabla ya mwisho wa mwezi huu. Tuliahirisha kidogo kwa kuwa imekuwa vigumu kupata majina wa waliojeruhiwa. ” aliongezea kusema mkuu wa ulinzi.
Jenarali Musa amesema taifa hilo la Afrika Magharibi linataka kutengeneza silaha wakati nchi nyingi zinasita kuiuzia silaha Nigeria kutokana na wasi wasi kuhusiana na haki za binaadamu. Hakuzitaja nchi hizo.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters .
Forum