Utekaji huo wa idadi kubwa ya watu katika jimbo la Katsina unasemekana ndio mkubwa katika mfululizo wa utekeji nyara wa hivi karibuni katika taifa hilo la Afrika lenye watu wengi.
Msemaji wa polisi Abubakar Aliyu amesema “wanawashuku majambazi wenye silaha kuvamia na kuwateka nyara wanawake 35” waliokuwa wakirudi kutoka harusi katika kijiji cha Sabuwa siku ya Alhamisi usiku.
Kamishna wa usalama wa jimbo Nasiru Muaz ametoa idadi kubwa zaidi ya watu walotekwa, akisema zaidi ya watu 50 wamechukuliwa walipokuwa wakirudi kutoka katika kijiji cha Damari baada ya kumsindikiza bi harusi nyumbani kwa bwana harusi.
Maafisa waliokitembelea kijiji hicho pia waliambiwa kuwa watu 53 walichukuliwa.
“Ilikuwa ni njia ya hatari sana ya kumpeleka bibi harusi kwa kuendesha gizani katika eneo kama hilo lenye ujambazi huku wakiimba kwa vifijo”
“Majambazi waliichukua nafasi hiyo na kuwateka” amesema.
Kamishna amewataka wakazi waepuke kusafiri nyakati za usiku na kusema waafisa usalama wanajaribu kuwaokoa mateka hao.
Utekaji nyara kwa ajili ya kulipwa fidia umekuwa tatizo nchini Nigeria. Kukiwa na magenge ya waharifu yakilenga barakara kuu, nyumba na hata kuwanyakuwa wanafunzi wakitoka mashuleni.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP.
Forum