Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, mjitoa muhanga kwa kwanza alijilipua kwenye sherehe za harusi mwendo wa saa 9 jioni, amesema mkurugenzi wa Idara ya dharura ya jimbo la Borno, Barkindo Saidu.
Dakika chache baadaye, mlipuko mwingine ulitokea karibu na hospitali, na kisha mwingine kwenye mazishi yaliokuwa yakiendelea. Watoto na wanawake wajawazito ni miongoni mwa watu waliokufa. Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika, ingawa kundi la Boko Haram lililioanza operesheni zake 2009, limekuwa likifanya mashambulizi kwenye mji huo, mara kwa mara.
Ghasia ambazo zimevuka mipaka kote kuzunguka ziwa Chad, zimeuwa zaidi ya watu 35,000, na kukosesha makazi wengine zaidi ya milioni 2.6, na kusababisha janga kubwa la kibinadamu. Boko Haram ambalo ni tiifu kwa Islamic State, limekuwa na lengo la kusimika utawala wa kiislamu nchini Nigeria, taifa lenye idadi ya watu takriban milioni 170, na ambalo limegawika kwa nusu, kati ya wakristo na waislamu.