Watu 24 wafariki katika mafuriko Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Mafuriko katika maeneo ya mashariki mwa Uganda yaliyotokana na mvua kubwa yamesababisha vifo vya takriban watu 24, serikali na shirika la msalaba mwekundu  Uganda zilisema.

Mafuriko katika baadhi ya maeneo ya Bugisu, Mbale na Kapchorwa awali yalisababisha vifo vya watu 10 siku ya Jumapili, wizara nchini humo inayosimamia misaada, maandalizi ya maafa na wakimbizi katika Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema katika taarifa yake Jumapili jioni.

Lakini idadi ya vifo iliongezeka zaidi leo Jumatatu.

Msemaji wa Msalaba Mwekundu wa Uganda Irene Nakasita aliwaambia waandishi wa habari kuwa kufikia sasa waokoaji wamechukua miili 21 kutoka Mbale na mingine mitatu kutoka Kapchorwa.

Alisema lori lililokuwa limebeba vifaa vya msaada lilikuwa njiani kwenda kuwahudumia waliopoteza makazi katika maeneo yaliyoathiriwa.