Shambulio hilo lilithibitishwa na mkazi mmoja wa eneo hilo pamoja na vyanzo vya usalama.
Burkina Faso, mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani, inapambana na uasi wa wapiganaji wa kiislamu ambao ulianzia nchini Mali mnamo mwaka wa 2015, na imeshuhudia zaidi ya raia 10,000, wanajeshi na polisi wakiuawa, kulingana na takwimu za shirika moja lisilo la serikali,
Takriban watu milioni 2 wamelazimika kuyahama makazi yao.
Hasira ndani ya jeshi kwa kushindwa kudhibiti uasi huo, zilisababisha mapinduzi mawili nchini Burkina Faso mwaka jana.
Mashambulizi manne ya watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi nchini Burkina Faso yaliwauwa wanamgambo 40 wa kujitolea, na wanajeshi 39 wa kawaida wiki iliyopita, jeshi na vyanzo vya usalama vilisema.
Mapigano mawili mabaya zaidi yalitokea katika eneo la Centre-Nord mnamo tarehe 26 mwezi Juni na taarifa za awali zilielezea kwamba darzani za watu walikuwa wameuawa.