Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:21

Burkina Faso yadai kufanyiwa hila na jumuiya ya kimataifa


Waziri wa ulinzi wa Burkina Faso, Jumatano ameshutumu kile alichokiita muungano wa kimataifa dhidi ya  nchi yake, na kushutumu kuwepo na ukiukwaji wa sheria za anga kwa nchi yake.

Pia idara ya ujasusi ya nchi hiyo imesema mauaji ya raia ya mwezi Aprili ambayo baadhi ya makundi ya haki za binadamu yamelishutumu jeshi, yalifanywa na wapiganaji wanajihadi waliovalia nguo kama wanajeshi.

Kanali Kassoum Coulibaly aliyeteuliwa na serekali ya mapinduzi inayotawala nchi kwa sasa, pia ameongeza kauli ya kupinga iliyotolewa na kiongozi wa nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traore kwamba mamluki wa kundi la Russia, Wagner walikuwa wakifanya operesheni zao Burkina Faso.

Amesema kwamba Russia ilikuwa haipangi mambo na haijatoa msaada wowote zaidi ya watu wa Burkina Faso ambao walikuwa wakichangia juhudi za vita kupambana na wanamgambo wanajihadi walioko nchini humo.

XS
SM
MD
LG