Unyanyasaji wa Kingono : Wanawake 15 wamtuhumu waziri India

Waziri aliye jiuzulu M.J Akbar,

Waziri mmoja nchini India amejiuzulu Jumatano kufuatia tuhuma kutoka kwa wanawake 15 wanaodai kuwa amewanyanyasa kingono wakati alipokuwa mhariri mkuu katika nafasi hiyo siku zilizopita.

M.J Akbar, Waziri mdogo wa mambo ya nje wa India, amekanusha kuwa hakufanya kosa hilo na amesema “atakabiliana na tuhuma hizo.”

Akbar alifungua mashtaka ya jinai Jumatatu dhidi ya Priya Ramani, mwanamke wa kwanza kati ya hao 15 kumtuhumu kwa udhalilishaji. Wanawake wengine 20 walisema wako tayari kutoa ushahidi wao dhidi yake mahakamani.

Hii ni moja ya kesi inayo mhusisha afisa wa ngazi ya juu iliyofungamana na harakati za kikundi cha kwenye mitandao #Me Too ambacho kimeendelea kupata nguvu.

Harakati hizi zilitia kasi na kujikita kupambana na unyanyasaji wa ngono ilipofikia mwisho wa mwezi Septemba baada ya mwanamama mchezaji filamu Tanushree Dutta kumtuhumu mchezaji filamu mwanamume Nana Patekar kuwa matendo wake haukuwa sahihi katika kundi la filamu zilizo tolewa 2008. Patekar amekanusha kutenda kosa lolote.