“Abiria hao walifyatuliwa risasi na gari hilo kuchomwa moto,” wakati wa shambulizi hilo lililofanywa na “magaidi” karibu na mji wa Bandiagara Ijumaa, maafisa wameiambia AFP.
“Serikali imetuma jeshi la usalama katika eneo la tukio,” wamesema, wakiongea kwa sharti wasitajwe majina yao.
Kiongozi aliyechaguliwa katika mji wa Bandiagara amethibitisha idadi ya vifo, akisema waathirika ni pamoja na wanawake na watoto.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi ambapo kuna makundi mbalimbali yenye silaha yanayofanya mashambulizi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Mali imekuwa ikijitahidi kudhibiti uasi wa vikundi vya Kiislam ambavyo vilizuka upande wa kaskazini mwaka 2012 na tangu wakati huo vimewaua maelfu ya wanajeshi na raia.
Pamoja na kuwepo kwa maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa, mgogoro huo umegubika maeneo ya katikati mwa Mali na kuenea katika nchi za jirani za Burkina Faso na Niger.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP