Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:13

Rais wa Marekani aiondolea vikwazo Burundi


Rais wa Marekani Joe Biden akielekea kwenye ndege ya Air Force One November 16, 2021 alipokuwa njiani kuelekea Woodstock, New Hampshire kuzungumzia muswaada wa miundombinu. (Picha na MANDEL NGAN / AFP)
Rais wa Marekani Joe Biden akielekea kwenye ndege ya Air Force One November 16, 2021 alipokuwa njiani kuelekea Woodstock, New Hampshire kuzungumzia muswaada wa miundombinu. (Picha na MANDEL NGAN / AFP)

Rais wa Marekani  Joe Biden leo amefuta  amri ya Taifa ya  kiutendaji dhidi ya Burundi  ambayo iliwekwa November 22 mwaka 2015 iliyohusisha pia  kuzuia mali za baadhi ya watu

Rais wa Marekani Joe Biden leo amefuta amri ya Taifa ya kiutendaji dhidi ya Burundi ambayo iliwekwa November 22 mwaka 2015 iliyohusisha pia kuzuia mali za baadhi ya watu.

Watu hao walichangia katika hali ilivyokuwa nchini Burundi ikiwemo mauaji na ghasia dhidi ya raia, vurugu, kuchochea ukandamizaji wa kisiasa vitendo ambavyo vilitishia amani ya nchi kwa kiasi kikubwa pamoja na ukosefu wa uthabiti katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na White House siku ya Alhamisi imesema kuwa baadhi ya hatua ambazo zilichukuliwa kabla ya amri ya dharura ya kiutendaji namba 13712 ya mwaka 2015 zitaendelea kuwepo, mpaka itakavyoamuliwa vinginevyo.

Amri hiyo ilizuia mali za watu ambao walisadikiwa kuhusika au kushiriki katika vitendo au sera ambazo zilitishia amani, usalama na uthabiti wa Burundi ikiwa ni pamoja na kudumaza mchakato wa kidemokrasia au taasisi mbali mbali nchini humo na kujihusisha na ukiukaji wa haki za binadamu.

Taarifa ya Biden imeelezea kwamba Marekani ina imani kuwa hali ambayo ilipelekea amri hiyo hivi sasa imeboreka na kuna umuhimu wa kuifuta amri hiyo.

XS
SM
MD
LG