Taifa hilo la Pembe ya Afrika limekabiliwa na uasi wa miaka 17 kutoka kwa kundi la Al-Shabaab, lenye uhusiano na Al-Qaeda, huku wanamgambo wa kundi la Islamic State pia wakiendesha shughuli zao nchini humo.
Siku ya Alhamisi, Ali Dahir, naibu mwenyekiti wa mahakama ya kijeshi ya Bossaso katika jimbo la Puntland, aliwahukumu Wamorocco sita kifo kwa kujaribu kuharibu maisha ya jamii ya Kiislamu, maisha ya watu wa Somalia na kusababisha uharibifu nchini humo.
Mahakama hiyo pia ilimuhukumu raia wa Ethiopia, na raia wa Somalia, kifungo cha miaka 10 gerezani kuhusiana na kesi hiyo hiyo.
Mwendesha mashtaka wa mahakama Mohamed Hussein aliwambia waandishi habari kwamba Wamorocco hao sita walikamatwa Puntland kufuatia uchunguzi ulofanyika kwa takriban mwezi mmoja.