Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:35

Pakistan: Operesheni kubwa ya msako inaendelea ikisaidiwa na jeshi


Vikosi vya usalama vikilinda nje ya hospitali huko Dera Ismail Khan, Pakistan.
Vikosi vya usalama vikilinda nje ya hospitali huko Dera Ismail Khan, Pakistan.

Mamlaka kaskazini magharibi mwa Pakistan zilisema Jumatatu kuwa shambulizi la kabla ya  alfajiri liliuwa maafisa wa polisi 10 na kujeruhi wengine sita kabla ya uchaguzi wa kitaifa baadaye wiki hii.

Shambulizi hilo limetokea huko Dera Ismail Khan kwenye mapambano ya wanamgambo ambako maafisa wanaripoti kuwa kikundi cha washambuliaji waliokuwa na silaha nzito walivamia kituo cha polisi, wakitumia bunduki za kushambulia kwa kuvizia na maguruneti na kuwashambulia maafisa wa usalama kwa risasi kabla ya kutoweka.

Polisi katika eneo walisema “operesheni kubwa ya msako” ilikuwa inaendelea hivi sasa kwa msaada wa wanajeshi wa Pakistani kuwasaka waliofanya mashambulizi. Barabara zote zinazoelekea ndani na kutoka nje ya wilaya hiyo zimewekewa vizuizi.

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na mauaji hayo, lakini wanaotiliwa ni Tehrik-i-Taliban Pakistan, au TTP, kikundi kilichopigwa marufuku ambacho kama kawaida yake hufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama katika wilaya hiyo iliyoko huko jimbo la Khyber Pakhtunkhwa linalopakana na Afghanistan.

Desemba mwaka jana, wanamgambo, wakiwemo wale washambuliaji wa kujitoa mhanga, walishambulia kituo cha jeshi huko Dera Ismail Khan, na kuuwa wanajeshi 23 na kujeruhi wengi wengine katika moja ya mashambulizi ya kinyama dhidi ya jeshi katika historia ya hivi karibuni ya Pakistan.

Shambulizi hilo lilidaiwa kufanywa na kikundi kipya kilichojitkeza cha wanamgambo kinachojulikana kama Tehrik-e-Jihad Pakistan, au TJP, kikiripotiwa ni tawi la TTP.

Makundi yote yanaendesha operesheni zake kutoka katika ardhi ya Afghanistan “kukiwa na uwezekano wa kusaidiwa na al-Qaida,” kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa wiki iliyopita.

Ongezeko la ghasia za wanamgambo limechochea wasiwasi wa usalama kwa wapiga kura na wanaoandaa uchaguzi wa bunge la Pakistan uliopangwa kufanyika Alhamisi.

Wafanyakazi kadhaa wa kisiasa, wakiwemo wagombea wa uchaguzi, wameuawa kwa mashambulizi ya bunduki na mabomu yanayotegwa na wanamgambo wakati taifa likielekea katika kupiga kura.

Forum

XS
SM
MD
LG