Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 15:12

Jeshi la Pakistan linasema wanamgambo saba wameuawa kusini mwa nchi hiyo


Jimbo la Baluchistan nchini Pakistan
Jimbo la Baluchistan nchini Pakistan

Taarifa ya jeshi imesema risasi pia zilipatikana baada ya shambulizi la kufyatuliana risasi katika jimbo la Baluchistan.

Jeshi la Pakistan limesema wanamgambo saba wameuawa Jumatatu katika mapambano ya risasi na vikosi vya usalama katika mkoa tete wa kusini magharibi mwa Pakistan, karibu na Afghanistan.

Taarifa hiyo fupi ya jeshi imesema kuwa risasi pia zilipatikana baada ya shambulizi la kufyatuliana risasi katika wilaya ya Zhob katika jimbo la Baluchistan. Gazeti la Dawn la nchini Pakistan, liliripoti kuwa silaha zilijumuisha bunduki, risasi na vilipuzi.

Wanamgambo katika mkoa huo wenye utajiri wa madini kwa miaka mingi wamekuwa wakitoa wito wa kushirikiana wa rasilimali za madini katika Baluchistan, lakini sasa wanatoa wito wa uhuru wa jimbo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG