Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 05:43

Imran Khan anyimwa nafasi ya kuwania urais wa Pakistan


Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan.
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan.

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan aliyefungwa jela Imran Khan pamoja na wafuasi wake kadhaa wamenyimwa nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi wa Februari 8, maafisa wa chama chake wamesema Jumapili, muda mfupi baada ya zoezi la kuandikisha wagombea kufungwa.

Khan amekuwa kuzuizini tangu Agosti akikabiliwa na kesi kadhaa ambazo anadai zina ushawishi wa kisiasa, ili kumzuia kuwania kwenye uchaguzi huo akiwa kama kiongozi wa chama cha Pakistan Tehreek e-Insaf, PTI. Kiongozi huyo aliyewahi kuwa nyota wa mchezo wa kriketi alikutwa na hatia ya ufisadi mapema mwaka huu, lakini mahakama baadaye ilisitisha kifungo chake cha miaka mitatu, wakati ikisikiliza rufaa iliyowasilishwa dhidi ya kesi hiyo.

Tume ya uchaguzi ya Pakistan, ECP ilimuondoa kwenye orodha ya wagombea kutokana na hukumu hiyo, lakini chama chake cha PTI kiliwasilisha stakabadhi zake za kuomba kugombea, mbele ya tume hiyo wiki iliyopita. Msemaji wa PTI Raoof Hasan ameiambia AFP kwamba tume hiyo kuwakataa wagombea ni njama ya kukizuia chama chao kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaofanyika katika muda wa wiki 6 zijazo.

Forum

XS
SM
MD
LG