Katika hatua tofauti Israel imeeleza bayana Jumapili kwamba hakuna Mpalestina ambaye atalazimishwa kuishi nje ya Gaza lakini kwamba vita vitaendelea.
Agenda ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken ilijaa mikutano ya ngazi ya juu katika dunia ya Kiarabu jana Jumapili kama sehemu ya juhudi zake za kupunguza mivutano na kuzuia kuenea kwa vita vya Israel na Hamas.
Mzozo wa karibuni ulianza wakati Hamas ilipofanya uvamizi wa kigaidi ndani ya eneo la Israel hapo Oktoba 7, na kuua takriban watu 1,200 na kuwachukua mateka watu 240.
Baada ya mkutano na mwenzake wa Jordan, Ayman Safadi, Blinkien alitembelea ghala ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani.
Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje, Marekani alisema: “Ni muhimu, muhimu sana kwamba tunapeleka misaada ya kutosha kwa watu wenye shida. Siyo tu kuwa tuipeleka Gaza na kuingia Gaza, lakini mara ikiwa iko Gaza, inatakiwa isambazwe kwa ufanishi kwa watu ambao wanaiihitaji kila mahali huko Gaza. Tutalifanyia kazi hilo katika siku zijazo pia.”
Mwanadiplomasia wa juu wa Marekani pia aliitembelea Qatar na kufanya mazungumzo an Waziri Mkuu Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.
Wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Blinken alikana taarifa za karibuni kuwa baadhi ya mawaziri wa Israel wametaka Wapalestina wapatiwe makazi mengine nje ya Gaza.
Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje, Marekani aliongeza: “Taarifa hizi si za kuwajibika. Zinachochea, na zinafanya mambo yawe magumu zaidi kwa musktabali wa wapalestina wanaoongozwa na Hamas huko Gaza ambayo haina tena udhibiti na makundi ya kigaidi ambayo hayana uwezo wa kutishia usalama wa Israel.”
Kufukuzwa kwa Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza siyo msimamo rasmi wa taifa la Kiyahudi, alifafanua Rais wa Israel, Isaac Herzog wakati alipoonekana katika kituo cha televisheni cha NBC katika kipindi cha “Meet the Press.”
Isaac Herzog, Rais wa Israel alisema: “Katika baraza lenye mawaziri 30, ambako siyo usalama wa baraza, waziri anasema chochote anachotaka kusema. Naweza nisipende, lakini hii ndiyo siasa ya Israel. Lakini nasema wazi kwa sauti kubwa, na rasmi na bila ya kusita, huu si msimamo wa Israel.”
Vita vya sasa havitamalizika, hata hivyo, mpaka malengo yote yamekidhiwa, alirejea kusema Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel alisema “Kutokomezwa kwa Hamas, kurejeshwa kwa mateka wote na ahadi kwamba Gaza haitakuwa tena tishio kwa Israel.”
Shinikizo linaendelea kuongezeka kwa Israel kulinda maisha ya raia wa Palestina na Blinken alisema atalizungumzia suala hilo, wakati wa majadiliano atakayofanya wiki hii nchini Israel.
Ripoti ya mwandishi wa VOA Veronica Balderag Iglesias.