Ziara ya mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani inafanyika wakati kukiwa na juhudi za kidiplomasia za upelekaji wa misaada ya kibinadamu kwenye Ukanda wa Gaza, pamoja na shinikizo kwa Israel kupunguza maafa miongoni mwa Wapalestina.
Baada ya kuwasili mjini Istanbul mapema leo, Blinken amekutana na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, pamoja na waziri wa mambo ya kigeni Hakan Fidan, wakati wakishauriana kuhusu nafasi ya Uturuki, pamoja na mataifa mengine ya kieneo, katika kupunguza taharuki iliyopo, pamoja na janga la kibinadamu linalohusishwa na vita vya Gaza.
Maafisa wa Marekani wameongeza kusema kwamba Blinkena anatarajiwa kushauriana na Uturuki kuhusu nafasi yake kwenye ujenzi wa Gaza baada ya mapigano.
Ziara ya Blinken ambayo ni ya 4 Mashariki ya Kati tangu Oktoba 7, inafanyika wakati vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas vikikaribia miezi mitatu.
Hamas limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na Marekani, Uingereza, na Umoja wa Ulaya, miongoni mwa wengine.
Forum