Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:01

Blinken afanya safari ya wiki nzima Mashariki ya Kati kuendeleza juhudi za kidiplomasia


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akielekea Mashariki ya Kati.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akielekea Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameondoka jana Alhamisi kwa safari ya wiki nzima huko Mashariki ya Kati akiendeleza  juhudi za  kidiplomasia za utawala wa Biden kuhusu  vita vya Israel na Hamas.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Vita hivyo vimedumu kwa miezi mitatu sasa, wakati khofu ya ghasia kuenea katika eneo ikiendelea kupamba moto.

Ziara hiyo inakuja kufuatia wasiwasi kwamba mzozo huo wa miezi mitatu unaenea mbali ya Gaza hadi Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel.

Pia kufikia vikosi vya Hezbollah kwenye mpaka wa Lebanon na Isarel, na kwenye njia za meli katika bahari ya sham.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje Mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani atasimama Israel, Ukingo wa Magharibi, Uturuki, Ugiriki, Jordan, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Misri .

Blinken atajadili hatua maalumu ambazo zinaweza kuchukuliwa na pande husika katika eneo ili kuzuia mzozo huo kusambaa.

Pia atajadili hatua za kuongeza misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Gaza na juhudi za kuwarejesha mateka wengine waliobaki ambao walitekwa na Hamas.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG