Israel imekaribisha habari za kuachiliwa mateka wawili wa Israel na Argentina ambao waliachiliwa na Israel leo lakini imesema mateka wengine waliobaki lazima waachiliwe.
Operesheni ya pamoja ya jeshi la Israel, Idara ya huduma ya usalama wa ndani ya Shin Bet na kitengo maalumu cha polisi huko Rafah iliwaachilia huru Fernando Simon Marman mwenye umri wa miaka 60, na Luis Hare mwenye umri wa miaka 70, jeshi limesema.
Wanaume hao wawili walitekwa na Hamas kutoka Kibbutz Nir Yitzhak Oktoba 7, jeshi limesema miongoni mwa matekani wengine 250 ambao Israel inasema walitekwa wakati wa shambulizi la kijeshi ambalo limechochea vita na Gaza.
Mateka hao wawili walioachiliwa wanatibiwa katika hospitali ya Sheba huko Israel, Mkurugenzi wa hospitali hiyo Profesa Arnon Afek amesema.
Mjini Tel Aviv ambako kumekuwa na maandamano ya mara kwa mara yanayotaka kuachiliwa mateka wa Hamas huko Gaza, Israel imesema inakaribisha habari hizo lakini nyingine zina hisia tofauti.
Wanamgambo wa Hamas waliuwa watu 1,200 kusini mwa Israel na kuteka wengine takriban 250 katika uvamizi wake wa Octoba 7.